Azam kuingia mtaani kusaka Vipaji


Timu ya Azam ipo kwenye mchakato wa kuanza kuingia mtaani ili kupata vipaji mbali mbali vya soka.

Azam kupitia msemaji wake Jaffar idd amesema kuwa zoezi hilo litaanza Agosti 28 mwaka huu katika Wilaya ya kigamboni na Temeke katika uwanja wa chamanzi.

Zoezi hilo pia litahamia Ilala ifikapo Septemba 3 katika uwanja wa JMK mwaka huu ambapo watamalizia kinondoni Septemba 10 katika uwanja wa kawe mwaka huu.

Aidha zoezi hilo pia litandelea nje ya mkoa wa Dar es Salaam katika mkoa wa Morogoro, Zanzibar, Tanga, Arusha, Mwanza na Kigoma.

Comments