Azam: Stars haitabadilisha ratiba yetu ligi kuu


Timu ya Azam FC imesema kuwa haitafanya mabidiliko yoyote ya ratiba ligi kuu licha ya kuwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wataungana na Timu ya Taifa katika mechi dhidi ya Nigeria Septemba 3 mwaka huu.

Azam kupitia msemaji wake Jaffar Idd wamesema kuwa TFF isihangaike na suala ya kutengua ratiba ya mechi hiyo dhidi ya Prisons ya Mbeya ambayo itachezwa Septemba 7 mwaka huu ikiwa ni siku tatu kupita baada ya kucheza Taifa Stars.

"Wachezaji wetu watakaotua watakaotua Tarehe 5 nchini watakatiwa tiketi za ndege ambazo zitawapeleka kwa haraka kuungana na wenzao mkoani Mbeya." Alisema Jaffar Idd

"Hatuna muda wa kupoteza, tunahitaji kwenda na ratiba kama ilivyopangwa tumalize mechi zote jijini Mbeya, dhidi ya Prisons na Mbeya City." Aliongeza msemaji

Azam ina kibarua kizito baada ya kumaliza mechi hizo ambapo msemaji huyo alisisitiza kuwa wanahitaji kwenda na ratiba watenge wiki ili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Simba ambayo itachezwa Chamanzi Complex.

"Tuna kibarua kizito cha kukabiliana na  Simba baada ya Mechi za Mbeya, hivyo tuna wiki nzima ya maandalizi ili kujiweka sawa kabla ya kukutana na Simba." Alisisitiza msemaji huyo.

Comments