Timu ya Azam leo itashuka dimbani katika mchezo wa kujipima nguvu na JKT Ruvu katika uwanja wa Chamanzi Complex.
Azam ilikuwa visiwani Zanzibar ambapo iliweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi chini ya mwalimu Zeben Hernandez na sasa wamerejea Dar es Salaam kukamilisha zoezi zima la usajili.
Afisa habari wa Azam Jaffar Idd amesema kuwa kocha ya timu hiyo anahitaji mechi nyingi zaidi za kupima nguvu kikosi chake pamoja na kuangalia wachezaji atakaowasajili.
"Kocha amepanga idadi ya wachezaji anaotaka kusajili ndani ya wiki hii atakabidhi majina hayo na kuachia uongozi kuendelea na suala zima la kukamilisha zoezi hilo." Alisema Idd.

Comments
Post a Comment