Kuna mabadiliko makubwa ndani ya kikosi cha Azam, jana niliona tofauti ya Azam ya Stewart Hall na mhispania Zeben Hernandez.
Azam ya Muingereza Stewart Hall ilipoteza radha ya ramba ramba. Ramba ramba huwa ina utamu na kawaida kwa maisha ya shule wanafunzi huipenda kutokana na utamu wake.
Nimeliona jibu la mabadiliko ndani ya Azam, pamoja na mfumo wa Zeben ule 3-5-2 vijana wa azam akiwemo Himid Mao wameonesha mabadiliko ndani ya mfumo huo.
Azam iliyopita ilikuwa nzuri lakini ilishindwa kutuliza na kutawala mchezo uwanjani kama ilivyokuwa kwa yanga ndiyo maana hakuna jambo la kwa Ndanda FC na JKT Ruvu kuchoma idadi ya goli 2 na kuyafanya matokeo kuwa sare pale Chamanzi.
Nadhan Hernadez anarudisha utamu wa ramba ramba pale Azam, anajua namna ya kubadilisha mchezaji leo Himid anatimia nguvu kwa maarifa anajua ni namna gani anapaswa kuhakikisha eneo la katikati linakuwa lao, na kucheza mpira wenye pasi za uhakika.
Stewart Hall ni kocha lakini nadhani alikaba zaidi lakini, hawakujenga wachezaji kuwa wenye kujiamini na kuchezea mpira ili kutuliza presha ya mashambulizi kutoka kwenye timu pinzani.
Nadhani ilikuwa rahisi kwa timu pinzani kama ndanda na JKT kuchomoa magoli kwa urahisi.
Naikubali URA kwa soka lao la uhakika na utulivu na ndio maana mara nyingi Simba iliangukia pua kwa waganda hao, nadhani Azam ilichagua timu sahihi ya kujipima nayo.
Naiona Azam mpya kwa Zeben Hernandez, ameanza kuongeza sukari ili mashabiki na wapenzi wa Azam wafaidi utamu wa ramba ramba, yenye ladha kamili ya ya ramba ramba.

Comments
Post a Comment