Baada ya ushindi mnono wa bao 2-0 waliopata Serengeti boys dhidi ya Afrika Kusini, kikosi hicho kinatafutiwa kambi nyingine tulivu zaidi.
Rais wa TFF Jamal Malinzi mwanzoni aliweka ahadi yake ya kuipeleka timu hiyo kuweka kambi nchini Madgascar kujiandaa na Afrika kusini ambapo alifanya hivyo.
Sasa huenda rais huyo wa TFF akaipeleka timu hiyo nje ya nchi ili kuwafanya kuwa na utulivu wa hali ya juu kwa ajili ya kupata matokeo bora zaidi kwenye soka.
TFF imejipanga kwa ajili ya kambi hiyo kilichobakia ni kufanya maamuzi ya mwisho kwa ajili ya kupata kambi yenye utulivu zaidi.
Serengeti boys inakibarua cha mwisho cha kufuzu fainali za kombe mataifa Afrika endapo itafanikiwa kuichomoa timu ya vijana ya Congo Brazaville ambapo septemba 16 Serengeti boys watakuwa wenyeji Dar es Salaam na marudiano yatakuwa Septemba 30 nchini Congo.

Comments
Post a Comment