Timu ya taifa ya Brazil kwa upande wa wanaume imeshindwa kutamba kwenye ufunguzi wa mashindano ya Olympic baada kukubali sare isiyokuwa na magoli dhidi ya Afrika Kusini.
Brazil ilishindwa kutamba mbele Bafana bafana ikiwa katika uwanja wa Estadio Nacional kutokana na safu nzuri ya ulinzi ya ilisukwa na Afrika kusini.
Kwa upande mwingine timu ya Algeria ilishindwa kutamba mbele ya Hondorus baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2.
Hata hivyo kikosi cha Algeria kina nafasi ya kujiuliza katika mchezo ufuatao itakapokutana na Argentina ambaye ndiye aliyekuwa mshindi wa medali dhahabu ambaye alipokea kichapo cha mabao 2-0 kwa vijana wa ureno.

Comments
Post a Comment