Bale akamua 2, Madrid ikiua 3 ugenini


Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale amezidi kudhihirisha ubora baada ya kutupia bao mbili katika ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Real Sociedad.

Bale alifunga bao la kwanza dakika ya 2 ya mchezo, Marco Asensio alifunga bao la pili dakika ya 40 na Bale alihitimisha furaha hiyo baada ya kutupia nyavuni bao la 3.

Hatua hiyo ni mwendelezo mzuri wa kocha wa sasa Zinedine Zidane ambaye anakubalika na nyota wengi waliopo Madrid kwa sasa.

Comments