Batshuay, Costa waibeba Chelsea


Washambuliaji wa Chelsea Mitchy Batshuay na Diego wamefunga magoli yaliwapa Chelsea ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Watford.

Watford walianza kupata goli kupitia Etienne Capoue aliyefunga kipindi cha kwanza hata hivyo Batshuay alichomoa bado kwenye dakika ya 80, na Costa kufunga la Ushindi dakika ya 90.

Chelsea imekusanya pointi 6 baada ya kuilaza West Ham katika mechi ya awali hali inayopelekea timu hiyo kuongeza kasi kwa wachezaji wake.

Comments