Timu ya Newcastle united jana imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 ikiichapa Reading katika uwanja wa nyumbani.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa Rafael Benitez ambaye alipoteza mechi mbili mfululizo ikiwemo ya kwanza dhidi ya Fulham na Huddlesfield.
Newcastle ilipata mabao hayo kupitia Isaac Hyden, Matt Ritchie aliyefunga kwa Penati na Dwight Gayle aliyefunga kwa mara mbili.
Benitez ana kibarua kigumu cha kuirudisha Newcastle ligi kuu kutokana na ushindani mkubwa uliopo ligi daraja la kwanza

Comments
Post a Comment