Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke amekalisha usajili wake akitokea Liverpool kwenda Crystal Palace kwa dau la £32 milion.
Benteke 25 amemwaga wino miaka minne kuitumikia Palace ambapo atakuwa na timu hiyo hadi 2020.
"Nimefurahi kutua Palace kukutana na wachezaji wa hapa, na maisha ya apa pamoja na uongozi mzima." Alisema Benteke.
Benteke anakuwa mchezaji wa nne kutua Palace baada ya kufanyika kwa usajili wa awali ukiwemo ule wa Andros Townsend, James Tomkins na Steve Mandanda.

Comments
Post a Comment