Leo katika ligi ya England Tottenham Hotspurs wataikaribisha Liverpool katika uwanja wa White Hart Lane ikiwa ni mechi ya tatu tangu kuanza kwa ligi.
Habari kwa Liverpool ni kurejea kwa Sadio Mane,Daniel Sturridge na Joel Matip ambao wote walikumbwa na majeraha lakini wako fiti kwa mchezo leo.
Kwa upande wa Spurs wako kamili na wachambuzi wengi wa soka wametupia karata kwa Spurs kuibuka na ushindi akiwemo Paul Merson aliyetabiri ushindi wa bao 2-1 kwa Spurs.
Kuna uwezekano mkubwa Spurs wakatalawa zaidi mpira kuliko Liverpool kutokana na safu ya kiungo ya Spurs kuwa imara zaidi.
Uwepo wa Mousa Dembele, Victor Wanyama, Delle Ali na Erickssen unaweza kuleta tabu kwa Liverpool, sababu kubwa ni kwamba Liverpool inakosa kiungo mkabaji wa kutuliza mashambulizi na kuisaidia safu ya Ulinzi.
Natarajia uwepo mdogo wa mwanya wa magoli kwa katika lango la Spurs kama Victor Wanyama na Moussa Dembele watuwa kwenye ubora wao.
Ingawa Liverpool ina udhaifu katika eneo la ulinzi lakini ni tishio katika safu ya kushambulia, uwepo wa Felipe Coutinho, Sadio Mane, Sturridge na Firmino ni hofu tosha kwa lango la Spurs. Nadhani mechi itakuwa na utamu wa aina yake.
Kwa misimu minne ya hivi karibuni nadhani Liverpool amekuwa mbabe kwa Spurs, Hasa ule wakati wa Brendan Rodgers aliwamudu ipasavyo.
Spurs ina kasi na Liverpool ina kasi, msimu uliopita walitoshana nguvu White Hart Lane na Anfield, sijui nani ataubuka mbabe msimu huu kati ya Mauricio Pochettino na Jurgen Klopp.

Comments
Post a Comment