Big Sam aanza na Michail Antonio


Kocha wa England Sam Allardyce ameanza harakati za kupata kikosi chake baada ya kuanza na Michail Antonio wa West Ham.

Antonio amewahi kuwa chini ya Big Sam wakati kocha huyo akiwa na timu ya West na ndiye kocha aliyemsajili nyota mwaka 2015.

Sam 61, anavutiwa na kiwango cha nyota huyo wa West Ham ambaye ndiye amefunga mara nyingi kwa kichwa kuliko mchezaji yeyote England tangu aliposajiliwa ligi kuu akiwa amefunga mara 8 hadi sasa.

Licha ya Antonio, huenda nyota mwingine wa West Ham ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo Mark Noble akaitwa kwenye kikosi cha England na kocha huyo.

Comments