Kocha wa sasa England Sam Allardyce anataka kumrudisha beki wa Chelsea John Terry kwenye timu ta taifa.
John Terry aliachana na timu ya taifa miaka 4 iliyopita baada ya kutuhumiwa kumbagua beki wa QPR Les Ferdinand ambaye ni mdogo wa aliyekuwa beki maarufu wa Manchester united Rio Ferdinand.
Mwaka 2011 Chelsea ilipoteza mechi dhidi ya QPR katika mechi hiyo John Terry alishikwa na hasira na kumbagua beki huyo, ambapo mwaka 2012 chama cha soka England (FA) kilimtoza beki huyo £ 22,000 kama faini na adhabu ya kufungiwa mechi.
Sam anaona John Terry ana umuhimu kwa sasa kwenye safu yake ya ulinzi lakini mpaka sasa hajafanya makubaliano yoyote na beki huyo.
Sam atachagua wachezaji wake rasmi ambao wataunda kikosi cha England ifikapo Septemba 28 mwaka huu.

Comments
Post a Comment