Mshambuliaji wa Crystal Palace Yannick yuko mbioni kutua Everton kwa dau la £30 milioni.
Bolasie ametua Merseyside kukamilisha zoezi la vipimo ambalo linafanyika leo ili baada ya Crystal Palace kuridhia ofa iliyowekwa mezani na Everton.
Bolasie 27, amekuwa tishio tangu alipotua England na Ronald Koeman ambaye ni kocha wa sasa wa Everton anataka kukamilisha dili hilo kuziba pengo la Romelu Lukaku ambaye anahusishwa na kurudi Chelsea.
Bolasie akiwa na Crystal Palace amefunga jumla ya mabao 13 katika 133 alizocheza akiwa na timu hiyo.

Comments
Post a Comment