Mwanariadha mwenye mbio Usain Bolt wa Jamaica usiku wa kuamkia leo ameiwezesha nchi yake kushinda mbio za kupokezana vijiti (4×100 relay) katika michuano ya olympic ya Rio.
Bolt, 29, akiwa na wenzake Nickel Ashmeade Yohan Blake, Asafa Powell wameshinds mbio hizo wakitumia muda wa sekunde 37.27 na kujinyakulia dhahabu huku Japan wakichukua ya fedha na medali ya Shaba ikienda kwa Canada baada ya marekani waliomiza nafasi ya tatu kunyimwa medali hiyo kwa kukosea kupokezana vijiti.
Bolt anakuwa mwanariadha wa kwanza kunyakua medali ya dhahabu mbio za mita 100, 200, 4×100 relay mara tatu mfulilizo katika michuano ya Olympic
Alinyakua medali hizo katika masindano yaliyofanyika Beijing 2008, London 2012 na Rio de Janeiro 2016, Triple-Treble.
"Mimi ni bora zaidi, ninafuraha na ninajisifu nimekamilisha malengo, niliwaambia wenzangu, kama hatutashinda hii ntawapiga" Alisema Bolt.
Hii ni medali yake ya 9 katika michuano ya Olympic na ni historia kubwa katika mashindano hayo na uenda ikawa michuano yake ya Olympic kushiriki.

Comments
Post a Comment