Bony atua Stoke city kwa mkopo


Wakati dirisha la usajili barani Ulaya likielekea ukingoni tayari mshambuliaji wa Manchester city Wilfrey Bony amekalisha dili lake la kutua Stoke city kwa mkopo.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la paundi 28 milioni akitokea Swansea January 2015, ameshindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Man city na hivyo kwenda kunoa makali yake Brittania chini ya kocha Mark Hughes.

Kwa upande wa mchezaji huyo amesema kuwa amefurahi kutua Stoke city na sasa yupo tayari kupokea changamoto mpya katika kikosi hicho.

"Nimefurahi, nimeridhika pia kutua kwenye timu na kuungana na wachezaji wa hapa hakika nipo tayari kupokea changamoto mpya na kuzoea maisha ya hapa." Alisema Bonny

Aidha kocha wa Stoke city Mark Hughes amesema amesema ana imani amepata mchezaji bora ambaye ataongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.

"Wengi wanamfahamu mchezaji huyu, ana uwezo mkubwa wa kufunga magoli, alifanya kazi kubwa Swansea nadhani atafanya hivyo pia katika timu hii." Alisema Hughes

Comments