Golikipa wa Chile Claudio Bravo sasa ni mchezaji rasmi wa Manchester city baada ya kusaini miaka minne kwa dau la uhamisho wa £15 milioni.
Bravo ndiye atakayekuwa kipa namba moja kwa sasa katika timu hiyo mbele muingereza Joe Hart pamoja na Muargentina Willy Caballero.
Kwa upande wa Bravo alisema ana furaha ya kujiunga na Manchester city pamoja na nia yake ya kuiletea timu hiyo mafanikio.
"Nina furaha ya kujiunga na timu hii, nadhani nitakuwa sehemu ya kuiletea mafanikio timu hii." Alisema Bravo
Bravo alijiunga na Barcelona mwaka 2014 na kufanikiwa kutwaa mataji mawili ya La liga pamoja na taji moja ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Comments
Post a Comment