Bravo huyoo Manchester city


Maisha ya mlinda mlango wa Manchester city Joe Hart yapo mashakani baada ya Barcelona kufikia makubaliano ya kumuuza Claudio Bravo Etihad.

Pep Gurdiola anahitaji Golikipa anayelandana na mfumo wake unaoanza kufanya kazi katika timu yake ya sasa.

Bravo 33, huenda akatua etihad muda wowote kuanzia sasa baada ya Barcelona kukiri wamefikia pazuri na Man city kwenye mpango mzima wa kumpiga bei kipa huyo.

"Ni kweli tumefikia makubaliano ya kumuuza Bravo, tuna imani tutapata golikipa mwingine makini kama yeye." Kilisema chanzo

Comments