Chadli ataua West Brom


Kiungo wa Tottenhma Hotspurs Nacer Chadli ametua katika timu ya West Brom baada ya kusajiliwa kwa dau la paundi 13 milioni.

Raia huyo wa Ubelgiji amesaini mkataba wa miaka miaka minne kuitumikia timu hiyo ambayo inanolewa na Tony Pulis hadi mwaka 2020.

Kiwango kizuri kinachooneshwa na Muargentina Eric Lamela pamoja na Delle Alli ndiyo sababu ya kuondoka kwa nyota huyo wa Ubelgiji ambaye ameshindwa kutamba kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Mbali na wachezaji hao, kocha wa Spurs Mauricio Pochettino ana imani kubwa na Eric Dier, Moussa Dembele na Victor Wanyama aliyesajiliwa kutoka Southampton ambao moja kwa moja wamemnyima mchezaji huyo hamu ya kuendelea kubaki White Hart Lane.

Comments