Timu ya Chelsea jana ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani ilianza ligi na ushindi baada ya kuichapa West Ham mabao 2-1.
Eden Hazard ndiye aliyeanza kufungua ukurasa wa mabao baada ya kufunga kwa penati kipindi cha pili.
West Ham ilichomoa bao dakika ya 67 kupitia beki wake wa kati Collins ambaye aliunganisha mpira uliotokana na kona fupi iliyopigwa na Dimitri Payet.
Hata hivyo Chelsea ilipata bao la pili dakika 89 kupitia Diego Costa aliyefunga kwa shuti kali baada ya mshambuliaji Mitchy Batshuay na kuyafanya matokeo kuwa 2-1 hadi mwisho wa mchezo.

Comments
Post a Comment