Timu ya Manchester city ikiwa leo katika uwanja wake wa nyumba imezidi kutanua mbawa zake baada ya kuifunga West Ham 3-1.
Manchester city ilifunga mabao hayo kupitia Raheem Sterling aliyefunga bao mbili na Fernandinho huku bao la kufutia machozi la West Ham lilizamishwa nyavuni na Mikhail Antonio.
Kama ilivyo kawaida ya Gurdiola Man city ilitawala zaidi mpira katika eneo la kiungo na David Silva alizidi kuwa meiba kwa wapinzani wake.
Hadi mpira unamalizika Man city ilikua imetawala mpira kwa asilimia 62 na 38 zilizobaki zilikuwa za West Ham.

Comments
Post a Comment