Conte amuweka Oscar sokoni


Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema kuwa yupo tayari kumwachia Oscar endapo Intermilan itafikia dau la £30 milioni.

Intermilan ipo kwenye mipango ya kumuuza mshambuliaji wao nyota Mauro Icardi katika timu ya Napoli na kocha wa timu hiyo Roberto Mancini anafikiria kufanya usajili wa nyota kadhaa akiwemo Oscar wa Chelsea.

Mbrazili huyo mwenye miaka 24, ameshindwa kumvutia kocha wa sasa Antonio Conte ambaye yupo na kikosi hicho kwenye ziara ya  kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Conte anafikiria kumuuza Oscar na kumrudisha Romelu Lukaku Chelsea ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ambayo inaonekana kupwaya.

Mbali na Oscar Chelsea pia inamweka sokoni Nemanja Matic atakua huru kuondoka endapo kuna timu itatoa ofa ya kumnunua mchezaji huyo ambaye anatolewa macho na juventus.

Comments