Kiungo wa England Danny Drinkwater amejifunga rasmi Leicester baada ya kusaini miaka mitano kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2021.
Drinkwater kwa sasa anaungana na Wes Morgan, Jamie Vardy na Rihad Mahrez ambao nao wamejifunga kwenye timu hiyo baada ya kusaini mkataba mpya.
"Ninaipenda timu hii, ninafurahi kwa kuwa nitaendelea kuwa apa kwa miaka mitano." Alisema Drink water
Kiungo huyo wa Leicester alichipukia katika timu ya vijana ya Manchester united kabla ya kupata umaarufu kwenye timu yake ya sasa.

Comments
Post a Comment