Dzeko, Salah waiua Liverpool


Liverpool imejikuta ikipoteza mechi ya pili baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya AS Roma.

Mabao ya AS Roma yalifungwa na Edin Dzeko ambaye alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 29, Salah aliyefunga goli la ushindi kunako dakika ya 62 licha ya kinda wa Liverpool Sheyi Ojo kuchoma bao moja kipindi cha kwanza.

Awali Liverpool ilipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Chelsea baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 wiki iliyopita katika hatua za kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Liverpool itakamilisha maandalizi hayo dhidi ya Barcelona Agosti 8 mwaka huu katika uwanja wa Wembley nchini Uingereza ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu England.

Comments