FIFA yaleta kozi ya Stamina Tanzania


Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limeipa nafasi Tanzania ya kutoa kozi maalum ya Stamina (Physical Fitness) kwa makocha wenye kiwango cha leseni B.
Kozi hiyo ambayo imeanza jana inatolewa na mkufunzi kutoka FIFA Dk. Praddit Dutta ambaye ni raia wa India.

Akifungua kozi hiyo katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesiga alisema anaishukuru FIFA kwa kutambua nafasi ya watanzania katika soka na kuwapatia fursa hiyo.

"Si kila nchi inaweza kupata fursa, ujue kwamba FIFA inafahamu maendeleo ya soka kwenye  nchi hii, na ndio maana tukapaitiwa fursa hii, FIFA inazunguka kila kona ya dunia lakini imefika Tanzania." Alisema Mwesigwa.

Kwa upande wa Dk. Dutta alisema kuwa Tanzania imepata fursa hivyo watakiwa kufanya vizuri kwa kuwa kozi zingine zinakuja

"Tanzania imefungua ukurasa mwingine kwenye soka, kwa upande wa makocha na waamuzi hii fursa ni kubwa mnatakiwa kufanya vizuri kwa kuwa kozi zingine zinakuja." Alisema Dk. Dutta.

FIFA kwa kushirkiana na idara ya ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya mkurugenzi Salum Midadi imechagua jopo la makocha 27 wenye Leseni B ambao wanashiriki kozi hiyo.

Comments