Genk ya Samatta rasmi Europa Ligi


Timu anayochezea nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta, KRC Genk imetinga hatua ya makundi ya ligi ya Europa.

Katika mchezo huo wa pili wa round ya tatu KRC Genk wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya wenyeji wao Cork City ya Jamhuri ya Ireland, mchezo huo ambao umechezwa katika uwanja wa Turners Cross nchini Ireland, goli la mapema lililofungwa na nahodha wao Thomas Buffel dakika ya 13 na Sebastien 
Dewaest dakika ya 41 zilitosha kumaliza mchezo na wenyeji wao

Cork City waliambulia goli moja lililofungwa na Alan Bennett dakika ya 63.
KRC Genk licha ya kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 katika mchezo wao wa awali uliochezwa Cristal Arena,  hivyo Genk wamesonga mbele kwa aggregate ya goli 3-1, sasa Genk watacheza  hatua ya Makundi ya michuano ya Europa League .

Comments