Ghana kujipima nguvu na Warusi, Septemba 6 mwaka huu


Timu ya Ghana itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Urusi jijini Moscow Septemba 6 mwaka huu.

Ghana itakuwa imepumzika kwa siku tatu tu itapocheza mechi hiyo kwa kuwa itacheza dhidi ya Rwanda Septemba 3 katika mechi ya kufuzu kombe la mataifa barani Afrika ambapo tayari timu hiyo imeshafuzu kuelekea Gabon mwaka 2017.

Pia kocha wa timu hiyo Avram Grant ataungana na Assamoh Gyan ambaye kwa sasa anakipiga katika timu ya Shanghai SIPG ambayo inashiriki Super League ya China.

Hata hivyo Ghana itamkosa mshambuliaji wa West Ham Andrew Ayew ambaye bado anasumbuliwa na majeraha zikiwa zimepita wiki 3 tangu alipoumia katika mechi ya Chelsea kwenye ufunguzi wa EPL.

Comments