Ni siku chache tangu ligi ya England imeanza lakini kocha wa sasa wa Manchester city Pep Gurdiola amepoteza imani na mlinda mlango namba moja wa timu hiyo Joe Hart.
Ingawa Gurdiola ametoa nafasi kwa golikipa namba 2 wa timu hiyo Willy Caberello lakini bado ana mipango ya kushusha kipa mpya Etihad.
Pamoja na kuwa kipa wa sasa wa England Joe Hart anachukizwa na jinsi kocha huyo anavyofanya, anataka kufanya maamuzi ya kuondoka kwenye timu hiyo.
Kuondoka kwa Joe Hart hakuumizi kichwa cha Gurdiola, kwa kuwa tayari yupo kwenye mipango ya kumleta Claudio Bravo wa Barcelona.
Gurdiola anataka soka la kumiliki na kutawala mpira, katika mfumo wake anahitaji kipa mwenye kujiamini atakayeanza kucheza mpira na mabeki kuelekea kwenye ngome ya wapinzani.
Ilikua hivyo kwa Victor Valdes ingawa watu walimuona ni kipa wa kawaida sana lakini alikuwa lulu kwa Gurdiola. Valdes alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza na mpira mabeki ata kiungo namba sita hii ndiyo Gurdiola anataka.
Wakati Gurdiola alipoanza maisha mapya na Bayern Munich alikutana na kipa bora zaidi duniani Manuel Neuer, nadhani hakuna shaka juu ya ubora wa kipa huyu ambaye anatikisa dunia kwa sasa.
Neuer anajiamini awapo uwanjani, ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, hili amelifanya ata Ujermani pia, na alifiti sana katika mfumo wa Gurdiola.
Hart amepoteza uwezo wa kujiamini uwanjani, bila shaka Gurdiola hana imani naye, anaona ni heri kuwa Cabellero kuliko kipa huyo.
Hakuna shaka Gurdiola ameamua kukimbilia polisi, ameamua kwenda Barcelona kupata kipa mwenye uwezo wa kuendena staili yake ya soka uwanjani. Bila shaka hawez kuumizwa iwapo kipa huyo England ataondoka.

Comments
Post a Comment