Gurdiola uso kwa uso na Barcelona


Pep Gurdiola amepata bahati ya kurejea katika dimba la Camp Nou wakati ambapo Manchester city itachuana na Barcelona kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Gurdiola ambaye ni kocha wa Manchester city amedondokea Kundi C ambalo yumo Barcelona, Borrusia Monchenglabach pamoja na Celtic.

Gurdiola anapata nafasi ya kuinusa Camp Nou kwa mara nyingine baada ya kufanyika hivyo mwaka juzi alipokutana na wababe hao wa Cataluny katika mchezo wa nusu wakati kocha huyo akiwa na Bayern Munich.

Comments