Golikipa wa England Joe Hart huenda akatimka Manchester city baada ya kocha wa sasa Pep Gurdiola kukosa imani na mlinda mlango uyo.
Hart 29, ameshindwa kumshawishi Gurdiola kutokana na kuonesha kiwango duni katika michuano ya UEFA Euro pamoja na mechi za kirafiki ikiwemo ile ya Arsenal.
Gurdiola hajamtumia kipa huyo kwenye mechi Mbili mfululizo ambazo Manchester city ilicheza ikiwemo ile ya ufunguzi wa EPL dhidi Sunderland na ile ya jana dhidi ya Bucuresti ambapo Willy Cabellero amekuwa chaguo la kwanza.
Kipa huyo amekuwa akifanya makosa ya wazi uwanjani na kuigharimu timu ikiwemo goli la pili ambalo England ilifungwa dhidi ya Iceland nchini Ufaransa na goli lingine alifungwa na Akpom wa Arsenal walipokutana kwenye mechi ya kirafiki.
Upo uwezekano wa kipa huyo kundoka kutokana na Gurdiola kutaka kumsajili raia wa Chile Bravo anayechezea timu ya Barcelona.

Comments
Post a Comment