Baada ya sakata la muda mrefu kuhusu usajili wa Laudit Mavugo hatimaye nyota huyo amewasili Simba jana.
Nyota huyo Vital O' ya Burundi ametua kimya kimya nchini ili kumalizana kabisa na Simba ikiwa ni pamoja na kuting rasmi uzi wa msimbazi.
Aidha Mavugo alihusishwa na mpango wa kwenda Ufaransa lakini sasa matumaini ya Simba yamerejea baada ya mrundi huyo kutua hapo jana.
Mavugo anakuwa strika wa tatu kusajiliwa na Simba msimu huu baada ya kufanya hivyo kwa Ame Ali na Blagnon kutoka Ivory Coast.

Comments
Post a Comment