Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard amesema kuwa ana imani ataanza vizuri ligi ya England chini ya konte msimu huu.
Hazard alifunga bao moja msimu uliopita alisema sasa anajiona kuwa bora chini ya Conte na kutamba kurejesha kiwango chake cha awali.
"Licha ya kocha kusajili wachezaji wawili lakini nina imani tutakuwa bora na tunakwenda kuanza vizuri chini ya Conte." Alisema Hazard
"Tangu nimetua Chelsea hii ni mara ya kwanza tumekosa champions ligi pamoja na europa lakini nadhani ni msimu mzuri chini ya Conte na tutafanya vizuri sana." Aliongeza Hazard
Hazard ameanza na kiwango kizuri katika mechi za maandalizi ya ligi, yakiwemo mabao mawili aliyofunga katika mechi dhidi Real madrid.

Comments
Post a Comment