Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Arsenal na mchambuzi wa Sky sports Thiery Henry ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa Roberto Martinez Ubelgiji.
Martinez ambaye aliondolewa na uongozi Everton alipata shavu la kuinoa timu ya taifa ya Ubelgiji baada ya Wilmot Kung'oka na Thiery Henry ndiye atakaye shirikiana naye.
Henry kwa upande wake ametoa shukrani kwa kocha Martinez na chama cha soka nchini kwa kumpa nafasi hiyo ya pekee.
"Nina mshukuru Martinez kwa mchango na chama cha soka nchini Ubelgiji hakika siwezi kukataa cheo hiki." Alisema Henry
Thienry ataungana na Martinez kuandaa Ubelgiji mpya ambayo hivi karibuni itashuka dimbani katika mechi za kufuzu kuelekea kombe la dunia.

Comments
Post a Comment