Kocha wa England Sam Allardyce ametangaza kikosi chake ambacho kitavaana na Slovakia kwenye mechi za kufuzu kuelekea fainali za kombe la dunia ambazo zitafanyika nchini Urusi mwaka 2018.
Kwenye kikosi hicho pia kimemjumuisha kiungo wa West Ham Michail Antonio ambaye ameitwa kwa mara ya kwanza England, pia Danny Drinkwater amerejeshwa kwenye timu hiyo.
Mshambuliaji wa Manchester united Marcus Rashford hajaitwa kwenye timu hiyo mpya ya England sababu pekee ya kocha huyo ni kuMtaka Mchezaji huyo aendelee kupata uzoefu kwenye soka.
Ifuatayo ndiyo orodha ya wachezaji wote ambao wanaunda kikosi cha Engand kwa sasa.
Mabeki: Cahil (Chelsea), Clyne (Liverpool), Jagielka (Everton), Rose (Tottenham), Shaw (Man utd), Smalling (Man utd), Stones (Man city), Walker (Tottenhma)
Viungo: Alli (Tottenham), Antonio (West Ham), Dier (Tottenham), Drink water (Leicester), Henderson (Liverpool), Lallana (Liverpool), Rooney (Man utd), Sterling (Man city), Walcott
Washambuliaji: Kane (Tottenham), Sturridge (Liverpool) na Vardy (Leicester city)

Comments
Post a Comment