Mshambuliaji wa timu ya Lyon ya Ufaransa Alexandre Lacazette amedhihirisha kuwa hashikiki kwa kufumania nyavu kwenye ligi Ufaransa baada ya kutupia goli 2 dhidi ya Caen jana.
Lyon imeendeleza safari yake ya ushindi ikiwa ni mechi ya pili mfululizo tangu ligi hiyo ilipoanza hivi karibuni.
Lacazette alifunga hat trick wiki iliyopita katika ushindi ambao Lyon ilipata wiki iliyopita dhidi ya Nancy na kuiwezesha timu hiyo kukusanya jumla ya pointi 6.
Lacazette anazidi kuumiza kichwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye anavutiwa na usajili wa nyota huyo ambaye aliachwa kwenye michuano ya Euro nchini Ufaransa.
Kabla ya kuanza kwa ligi ya Ufaransa Uongozi wa Lyon ulikanusha kuwa haukupokea ofa yoyote kutoka Arsenal kama ilivyodaiwa na vyombo vya habari kuhusiana na uhamisho wa Lacazette.

Comments
Post a Comment