Timu ya Intermilan imeachana na kocha mkuu Roberto Mancini ambaye amedumu kwa msimu mmoja.
Mancini 46, amekosa kuwa na maelewano na wamiliki wapya wa timu hiyo Suning jambo ambalo limepelekea kuondolewa kwa kocha huyo.
Intermilan sasa ipo kwenye hesabu ya kumleta aliyekuwa kocha wa Ajax msimu uliopita Mholanzi Frank De Boer ambaye pia yupo kwenye mipango ya Borrusia Monchenglabach ya Ujermani.
Hii ni mara ya pili Roberto Mancin anaondolewa Intermilan baada ya Inter kufanya hivyo mwaka 2008, na baadae kocha alipata kibarua Manchester city ambako alidumu kwa miaka 3.

Comments
Post a Comment