Beki wa Newcastle Daryl Janmaat amesaini Watford kwa uhamisho wa £7 milioni.
Muholanzi huyo mwenye umri wa miaka 27 amesaini miaka minne kuitumikia
Watford hadi mwaka 2020 akifuata nyayo za Giorginio Wijnaldum pamoja na Andros Townsend ambao pia wameondoka St James.
"Nimefurahi sana kutua Watford, walikuwa na imani na mimi ndiyo maana wamenisajili nina imani tutafanya vizuri." Alisema Janmaat
"Hakuna mchezaji asiyependa kucheza ligi kuu, nimekuwa nikitamani ligi kuu nina faraja kurejea ligi kuu." Aliongeza janmaat.

Comments
Post a Comment