Jembe letu limetubeba Afrika, linatuinua Ulaya


Wakati fulani nilikuwa na matumaini na Haruna Moshi Boban wakati ule amefanikiwa kuingia Gefle IF ya Sweden lakini nilishangazwa na kurudi kwake nyumbani bila kutengeneza jina Heshima.

Niliumia kuona kipaji cha kinapotea kwa kwa sababu ya kupenda uhuru wa maisha ya nyumbani, lakini nikajifariji inawezekana akaja mmoja wa watanzania akatuinua katika medali.

Wakati ule Victor Wanyama anaiua  Barcelona katika mechi za makundi champions ligi akiwa na Celtic nilipata wivu kwanini hatujatoa mtu kama wanyama hapa Tanzania.

Leo tuna mtanzania ananyata kama Wanyama, alianza na tuzo za Afrika, na watanzania tukaona fahari kupata kipaji kilichotoa heshima kwa watanzania.

Leo hii Mbwana Samatta anaongoza jahazi la Genk na wanatinga kwenye hatua ya makundi Europa ligi, akiwa na zaidi ya goli 3 alizoifungia Genk kuelekea makundi.

Samatta ameonesha na kuitangaza thamani yake Genk, ametoka kwenye nchi isiyovuma sana kwenye medani ya soka, lakini sasa Ubelgiji wanaanza kuijua Tanzania kupitia hili jembe letu.

Leon Bailey ambaye ambaye anafunga sana zaidi ya Samatta amepata rafiki bora ambaye anaziona nyavu kwa pamoja walitoa pigo zito kwa NK Lokomotiva na kutinga kwenye makundi ya europa ligi.

Sioni wivu tena juu Victor Wanyama kwa sababu jembe letu linaonesha mwanga na matumaini kwa waafrika na watanzia sitashangaa kama nitamuona La liga, League 1, Serie A au Bundesliga.

Nahodha wa taifa stars anatukumbusha tusibweteke kuna nafasi ya kutoka na kufanya vizuri endapo tutajituma na kupambana.

Samatta anastahili mafanikio kwa kuwa anajituma na kupambana hajaridhika na kubweteka kama Haruna Moshi 'Boban' hakika tumepata jembe, anatuinua Tanzania anatuniua Ulaya.

Comments