Kipa wa Manchester city Joe Hart amepanda ndege kwende Italy ili kufanyiwa vipimo na timu ya Torino ambayo atajiunga nayo kwa mkopo.
Hart 29, ameamua kuchukua hatua hizo kutokana na ujio wa golikipa Claudi Bravo ambaye anaonekana ndiye chaguo namba moja la kocha Pep Gurdiola kutokana na aina ya mfumo unaotumika kwenye timu hiyo kwa sasa,
Wakala wa mchezaji huyo Jonathan Barnett alikaliliwa akisema kuwa Hart atachezea Torino kwa sasa na tayari Manchester city imeridhia mpango huo.
Hart aliwahi pia kutolewa kwa mkopo katika timu ya Birmingham city, akiwa huko kiwango chake kilipanda maradufu ambapo aliweza kumwondoa golini wakati huo aliyekuwa kipa namba moja wa Man city na kipa wa sasa wa Stoke city Shy Given.

Comments
Post a Comment