Joel Campell atua Lisbon kwa mkopo


Mshambuliaji wa Arsenal Joel Campell ametua Sporting Lisbon ya Ureno kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Joel 24, ameshindwa kuingia kwenye timu ya kwanza ya Arsenal licha kuonekana kuimarika alipokuwa akiitumikia Villareal kwa mkopo.

Uwepo wa Theo walcott, Oxlade Chamberlain na Alexis Sanchez unamnyima mshambuliaji huyo wa Costa Rica fursa ya kutamba Emirates.

Licha ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha Professa Wenger nyota huyo ameendelea kuwa mchezaji wa kudumu kwenye taifa lake.

Comments