Kane: nitacheza Spurs ziku zote


Mshambuliaji wa Engand Harry Kane amesema anahitaji kubaki na Tottenham katika kipindi chote cha maisha yake ya soka mpaka atakapostaafu.

Kwenye mahojiano na Sky sports Kane alisema kuwa kwa sasa ni mchezaji mwenye furaha sana, na hivyo hana sababu ya kucheza soka nje ya timu hiyo.

"Nina furaha na maisha ya hapa nataka kupata mafanikio kupata mafanikio nikiwa na Tottenham." Alisena

"Sikuwahi kuweka mipango ya kuondoka, na wala sitaondoka Spurs, nataka kucheza hapa kwa kipindi chote hadi nitakapo staafu rasmi soka." Aliongeza

Licha ya kushindwa kwenye michuano ya UEFA Euro nchini Ufaransa lakini Kane 23 ndiye aliyekuwa mfungaji bora England baada kutupia nyavuni magoli 25.

Comments