Klopp awachimba mkwara Liverpool


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameonya wachezaji wake kuwa wasibweteke baada ya kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Barcelona.

Liverpool jana katika uwanja wa Wembley ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Barcelona ikiwa ni sehemu ya mwendelezo kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya EPL.

Klopp alisema wachezaji wanatakiwa kuongeza bidii kwa kuwa wana safari ndefu mbele huku akisisitiza kuwa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi.

"Barcelona timu kubwa na huu ushindi mkubwa kwetu, mashabiki wametusapoti kwa wingi nadhani tunatakiwa kuongeza bidii." Alisema Klopp

Liverpool itamaliza ziara yake Agosti 13 dhidi ya FC Mainz ya Ujermani kabla ya kutua Emirates dhidi ya Arsenal Agosti 13 katika ufunguzi wa ligi ya EPL.

Comments