Klopp: Sturridge ni tumaini langu


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema bado ana mipango na mshambuliaji Daniel Sturridge katika safu yake ya ushambuliaji.

Licha ya Sturridge kupatwa na majeraha ya mara kwa mara lakini bado Klopp ana imani kubwa na mchezaji huyo ambaye amekuwa mkali wa kufumania nyavu tangu alipotua Liverpool.

"Siwez kumfananisha na Sturrigde aliyekuwa anaingia Liverpool wakati huo lakini bado ana uwezo mkubwa kufunga magoli." Alisema Klopp

"Bado ana kasi kubwa na anaweza kufanya mambo makubwa uwanjani nadhani hakuna asiyefahamu mchango wa Sturrigde kwenye timu hii." Aliongeza Klopp

Liverpool imesafiri jana kwa ajili ya mechi dhidi ya Burton Albion na Klopp ameweka wazi kuwa Sturridge ataanza kwenye kikosi cha kwanza.

Comments