Kuelekea mchezo wa Yanga Jumamosi, Viingilio vyatajwa


Jumamosi ya wiki hii Yanga itamalizana na MO ikiwa ni raundi ya pili kwenye hatua ya na makundi wana jangwani hao wakiwa wenyeji wa timu hiyo.

Katika mchezo huo ambao utachezwa uwanja wa taifa, bei ya viingilio imepangwa kama ifuatavyo; shilingi 3000, kwa viti vya kijani, wakati viti vya orange na bluu eneo B na C gharama yake itakuwa shilingi 10000 wakati VIP A gharama yake ni shiling 15000.

Yanga ina pointi 1 na imebakiza jumla ya michezo miwili ukiwemo wa jumamosi dhidi ya MO Bejaia na TP Mazembe ambao utakuwa mchezo wa mwisho.

Yanga inatakiwa kupata ushindi ili kurejeha matumaini ya kusonga mbele. Kufungwa au sare ya aina yoyote itayeyusha kabisa matumaini ya Timu hiyo kuelekea nusu fainali.

TP Mazembe inakutana na Medeama ikiwa na pointi 10 kibindoni, Medeama yenye Pointi 5, MO Bejaia pointi 5 na Yanga ipo mkiani kwa pointi 1.

Comments