Leroy Sane asaini Man city


Timu ya Manchester city imekamilisha usajili wa kiungo Leroy Sane kutoka Schackle 04  kwa dau la paundi milion 37.

Sane 20, amesaini miaka 5 ya kuitumikia timu hiyo baada ya kuondoka rasmi kwenye timu yake ya Schackle 04.

"Ni mchezaji mzuri ambaye ana mbinu uwanjani, anajiamini akiwa na mpira mguuni kwake na mara nyingi napendezwa na jinsi anavyocheza mpira uwanjani." Alisema kocha Pep Gurdiol

"Yuko haraka na hutengeneza pasi nyingi uwanjani, anajituma zaidi na ni mfungaji wa magoli pia." Aliongeza kocha huyo.

Sane aliiongoza timu ya Ujermani katika hatua ya nusu fainali nchini Ufaransa, na amefunga magoli 8 katika mechi 33 kwenye ligi ya Bundesliga akiwa na Schakle 04.

Comments