Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) inaanza kutimua vumbi leo ambapo kuna mechi zitachezwa.
Simba ikiwa mwenyeji leo itaikaribisha Ndanda ya Mtwara katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, na Azam wataikaribisha African Lyon katika uwanja wa Chamanzi Complex.
Mkoani Shinyanga timu ya Stand United wanaikaribisha Mbao FC iliyopanda daraja msimu huu, lakini pia Wenyeji Mtibwa Sugar wanaikaribisha Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Maji maji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kutoka Mbeya kila moja ikiwa sawa kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu.
Mechi ya Yanga imesogezwa mbele hadi Agosti 31 mwaka huu kutokana na kuingiliana kwa ratiba ya kombe la shirikisho ambapo Yanga leo wanasafiri kuelekea nchini Congo kuivaa TP Mazembe katika mechi ya mwisho ya makundi.

Comments
Post a Comment