Liverpool yaangukia pua kwa Burnley


Baada ya kupata ushindi dhidi ya Arsenal leo Liverpool imeangukia pua baada ya kufungwa bao 2-0 na Burnley.

Burnley ilifunga magoli hayo kupitia Sam Vokes aliyefunga bao la kwanza na lile la pili likiwekwa nyavuni na Andry Gray aliyefunga kwa shambulizi la kushtukiza.

Liverpool ilitawala mpira kwa muda mrefu lakini ilikosa umakini kwenye safu ya ulinzi, pia Liverpool ilipwaya kwenye safu ya ushambuliaji.

Hata hivyo nidhamu ya mpira iliwabeba Burnley ambao walilinda lango lao vizuri na matokeo kubaki 2-0 hadi mwisho wa wachezaji.

Comments