Liverpool yaichapa Arsenal ugenini


Timu ya Liverpool imeibuka kifua mbele na kuchukua pointi 3 katika uwanja wa Arsenal (Emitares) baada ya kuifunga mabao 4-3.

Arsenal ilianza kupata bao kupitia Theo Walcott kipindi cha kwanza ambapo Phelipe itCoutinho wa Liverpool alichomoa bao hilo kwa mpira wa adhabu.

Kipindi cha pili Liverpool ilianza kwa kasi na kupata magoli matatu kupitia Coutinho aliyefunga bao la pili, Adam Lallana na Sadio Mane.

Hata hivyo Arsenal ilipata mabao mawili kupitia Oxlade Chamberlain na Chambers na kuyafanya matokeo kuwa 4-3 hadi mwisho wa michezo.

Comments