Liverpool imeshindwa kutamba mbele ya Tottenham Hotspurs baada ya kutoka ya bao 1-1 katika uwanja wa White Hart Lane.
Liverpool ndiyo walianza kupata bao la ushindi kupitia James Milner aliyefunga kwa mkwaju wa Penati dakika ya 42 ambapo Danny Rose alichomoa bao hilo dakika ya 72 ya mchezo.
Klopp amekosa ushindi kwa mara ya pili baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Burnley na kutoa sare mechi ya leo.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Liverpool kukusanya jumla ya pointi 4, na Spurs ikiwa na pointi 5.

Comments
Post a Comment