Liverpool yakataa ofa ya Benteke


Timu ya Liverpool imekataa ofa ya £23 milioni iliyowekwa mezani na Crystal Palace kumsajili Christian Benteke.

Kocha wa Palace Alan Pardew anataka kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji baada ya kumuuza Yannick Bolasie kwenda Everton pamoja na Gayle aliyetimkia Newcastle.

Crystal Palace imetoa imetenga kiasi hicho kama dau la awali bado ipo kwenye mipango ya kuongeza £7 milioni ili kuishawishi Liverpool kumuachia mshambuliaji huyo.

Benteke alisajiliwa Liverpool na Brendan Rodgers ambaye kwa sasa ni kocha wa Celtic kwa dau £32.5 akitokea Aston Villa.

Hata hivyo mbelgiji huyo ameshindwa kumshawishi Jurgen Klopp kamtumia katika kikosi chake cha kwanza kutokana na aina yake soka la pasi za haraka na spidi.

Comments